

Tena – alipewa miezi 12 ya kujirekebisha – lakini alipuuzia – na wala hakuitumia nafasi hiyo – na matokeo yake yote aliyoyaona kwenye ndoto, yalimtokea katika maisha yake!Kwa kuipuuzia ile ndoto, Mfalme Nebukadreza aliingia kwenye adhabu ya maisha yake, na afya yake kuvurugika kwa nyakati saba au miaka 7! Na pia “nafasi” yake ilikosa uongozi kwa miaka 7! Lakini pia kwenye ndoto ile aliyoota, alipewa maelekezo ya mambo ya kufanya, ili aliyoyaona kwenye ndoto yasimpate – lakini alipuuzia! Soma Danieli 4:27. Na ndoto ile ilimpa pia kujua adhabu atakayopewa asipobadili mwenendo wake. Ndoto ile – ilikuwa inampa onyo mfalme Nebukadreza, juu ya mwenendo wake aliokuwa nao wakati ule. Mfano wa pili: Danieli 4:1 – 34 tunaelezwa madhara yaliyompata mfalme Nebukadreza, kwa sababu aliipuuzia ndoto aliyoota! Je, umewahi kujiuliza ingekuwaje kama Farao angezipuuzia zile ndoto? Ni dhahiri ya kwamba angezipuuzia – angeona tu baada ya miaka saba njaa kali yenye kudumu miaka saba – huku hajajiandaa nayo!Na kwa vile njaa ile ilikuwa ni ya “dunia yote” (Mwanzo 41:56,57), ina maana dunia yote ingekumbwa na njaa, kwa sababu tu ya Farao kuzipuuzia ndoto – ikiwa angeamua kuzipuuzia zile ndoto! Na hata njaa ilipotokea miaka 7 baadaye haikuwasumbua – kwa kuwa ujumbe wa ndoto uliwapa kujiandaa. Na Farao akatekeleza maelekezo aliyopewa. Yusufu alimtafsiria zile ndoto na kumpa maelekezo yaliyoambatana na ndoto zile. Lakini biblia inasema, “asubuhi roho yake ikafadhaika” (Mwanzo 41:8) ikiwa ni kiashiria chenye ujumbe toka kwa Roho Mtakatifu, kwamba asizipuuzie ndoto zile! Asante Yesu hakuzipuuzia, na akatafuta msaada, ili ajue tafsiri yake. Hii ikiwa na maana ya kwamba wazo la kwanza lililomjia moyoni mwake, baada ya kuamka usiku ule, ni kuzipuuzia zile ndoto – na wala asiwe na mpango wa kuzifuatilia. Na zilikuwa na ujumbe mmoja uliofanana, uliokuwa unamjulisha ujio wa njaa nchini Misri miaka 7 baadaye – tokea wakati ule alipoota zile ndoto.įarao alipoamka alijisemea moyoni mwake ya kuwa: “Kumbe ni ndoto tu” (Mwanzo 41:7). Ndoto zile mbili zilikuwa na tafsiri moja iliyofanana. Mfano wa Kwanza: Unaposoma kitabu cha Mwanzo 41:1 – 7, unaona ndoto mbili alizoota Farao, kwa usiku mmoja, na kwa kufuatana. Jambo la 1: “Usiipuuzie ndoto uliyoota hata ikiwa hukijui chanzo cha ndoto hiyo!” Leo nataka nianze kukufundisha juu ya: “Mambo unayohitaji kuyajua kuhusu ndoto unazoota ili iwe vyepesi kufanikiwa kimaisha”.
